Islamic Calender

Powered by Blogger.

MU'TA NDOA YA HARAMU


Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu,bwana wa viumbe wote,na reh'ma na amani zimfiukie Mtume wetu Muhammad bin Abdillahi mbora wa viumbe wote,na ziwafikie jamaa zake na wake zake,na maswahaba zake wote kwa ujumla.
Ama baada ya utangulizi;
Jambo la familiya ni katika mambo muhimu sana,katika jamii ya kiislamu,na ndiyo maana Qur'ani imelizungumzia jambo hili katika pande zote,na Sunna ikasherehesha,na kufafanua na kuelezea kwa undani zaidi makusudio hayo ya Qur'ani.
na katika mambo muhimu yaliyo fafanuliwa kwa uwazi katika  Qur'ani na Sunna ni nidhamu kamili ya familia,
Qur'an na Sunna zimebainisha nidhamu hiyo kwa mpango ufuatao;
1- Qur'an na Sunna zimebainisha malengo matukufu ya ndoa.
2- mahimizo juu ya ndoa.
3- sifa za mume/mke mwema.
4- taratibu za kufanya iwapo utakosekana uwezo wa kuoa.
5- taratibu zote za kutimiza suala la ndoa.
6- haki za mke na mume,na wajibu wa kila mmoja.
7- namna ya kuyalinda mahusiano ya ndoa kati ya mke na mume.
8-mtazamo juu ya familia kabla ya uislamu na baada ya uislamu.
9- na suala la kuoa zaidi ya mke mmoja.
hukumu hizi zote zimefafanuliwa vizuri katika Qur'ani na Sunna kwa ufafanuzi wa wazi kabisa,tena ulio kamilika.
hivyo basi hakuna suala lolote katika hukumu za ndoa linalo hitajika halafu likawa halina ufafanuzi wa kisheria,
kwa mantiki hiyo basi,itakuwa haingii akilini kabisa,kuwa eti Qur'an na Sunna zimeruhusu Mut'a,halafu hakuna ufafanuzi wowote ule juu ya suala hili,kuanzia suala la kuwepo walii katika kufungisha ndoa,mashahidi hadi kufikia suala la kurithiana au kutokuwepo,
tena ndoa yenyewe iwe imehalalishwa kwa ishara ya mbali kiasi ambacho mpaka hao maulamaa wa tafsiri wenyewe hawaja wafikiana juu ya maana ya Aya hiyo,kama tutakavyo elezea hili mahala pake.
na wala hakuna tafsiri yoyote kutoka kwa Mtume (s.a.w.) inayoelezea kwamba Aya hiyo maana yake ni ndoa ya Mut'a, wala hakuna hadithi yoyote sahihi inayo bainisha hukumu,na taratibu za ndoa hiyo,si kwa ujumla wala kwa taf'sili !!
matokeo yake ndiyo wakajitokeza baadhi ya watu kwasababu ya tamaa,na matamanio ya nafsi zao wakaamua kutunga sheria zao kutoka akilini mwao.
na hilio ni baada ya kukosa katika kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wake (s.a.w.) upambanuzi yakinifu juu ya suala zima juu ya ndoa ya Mut'a !
ndiyo ukawa unawasikia wale wenye kuihalalisha ndoa hiyo haramu (kama Omar Mayunga na Abdillahi Nassir)
wakisema kuwa;
-Ndoa ya Mut'a haihitaji kusimamiwa na walii !
swali; je,ni kwa aya gani au kwa hadithi ipi ya Mtume Muhammad (s.a.w.) iliyojuzisha hilo?
au ni maoni binafsi?
je,hao walio jiwekea sheria hiyo wana nafasi gani katika dini hii ya kutunga sheria wazitakazo wao?
Allah anasema;
فانكحوهن بإذن أهلهن ....
(waoeni hao wanawake kwa idhini ya mawalii zao....) al maida aya 25.
na Bwana Mtume (s.a.w.) anasema;
Mwanamke yoyote atakaye jiozesha mwenyewe,bila idhini ya walii wake,basi mwanamke huyo ni mzinifu).
na katika riwaya nyingine inasema;(basi ndoa hiyo ni batili..).
huwenda watetezi wa ndoa hii ya haramu wakasema;
hiyo ni hukumu ya ndoa za kudumu,lakini Mut'a ina hukumu tofauti na ndoa hizo...
swali hukumu kaziweka nani? kwa ushahidi gani?
na ama kauli ya mwanawachuoni yoyote iliyo kinyume na kauli ya Allah na Mtume wake (s.a.w.) haitokubalika,na hukumu hiyo itakuwa ni batili kwa kuhalifu kauli ya Allah na Mtume (s.a.w.).
pia mtawasikia wakisema;
Ndoa ya Mut'a haihitaji kuwepo mashahidi !!
na hali ya kuwa Mtume (s.a.w.) anasema;
hakuna ndoa -itakayo sihi- bila ya walii na mashahidi wawili.
ameipokea hadithi hii Imam Ahmad katika musnadi yake,tazama Ir'waul ghalil juz 6/258-261.
pia mtawasikia wakisema;
Hakuna kurithiana -baina ya mke na mume katika ndoa ya Mut'a- anapokufa mmoja wao!
tazama kitabu Mut'a ndoa sahihi cha Mayunga uk 2.
na bila shaka hukumu ya Allah na Mtume wake ni tofauti na hukumu hii ya kina Mayunga,amesema Allah (s.w.t.);
(N a nyinyi mtapata nusu ya walichoacha wake zenu....)
na amesema kuhusu wanawake;
(nao -wake zenu- watapata robo ya mlicho kiacha...).
na hukumu hii ndiyo asili katika ndoa,kuwa wanandoa wanarithiana,na ila kitakapo patikana kizuwizi chochote cha kisheria kitakacho zuia kurithiana,kama vile;
mke kumuua mumewe au mume kumuua mke,muuaji hatomrithi mwenziwe.
au mmoja wao kuwa ni mtumwa,aliye mtumwa hatorithi.
au tofauti za dini,
na ama Mut'a ni kinyume kabisa na ubainifu huu wa Mtume (s.a.w.) hakuna katika ndoa hiyo ya haramu kurithiana kabisa, ni mamoja kuna sababu au hakuna ! na hukumu hiyo si Allah wala Mtume (s.a.w.) bali ni hukumu ya kina Mayunga na kundi lake,ndiyo pale wanapo hojiwa; ni ndoa gani basi hiyo isiyo na walii,mashahidi,wala kurithiana? badala ya kutoa ushahidi wa Qur'ani au Sunna sahihi za Mtume (s.a.w.) utawaona wanakwenda mbio huku wakitweta huku wakisema;
mbona Abu Hanifa kasema kwamba ndoa bila ya walii yafaa?!
Ibin Mundhir kasema haikuthibiti habari yoyote (sahihi)katika kushuhudia ndoa... !!
لاmwanamke wa ah'lulkitabi aliyeolewa na mwislamu,hawezi kumrithi mumewe...!!
hayo ndiyo majibu yao,badala ya kutoa hoja na dalili,wao hutumia ujanja ujanja katika dini.
sisi tunasema kwamba;lau kama Mut'a ni ndoa halali basi sheria ingebainisha hukumu zake,a-z,na wala isengehitajia ujanja ujanja wakina Mayunga na kaumu yake.
kama Abu Hanifa amesema kwamba ndoa bila ya walii inafaa,swali je Mtume (s.a.w.) anasemaje -ukiwa unamuamini-?



hoja zao za kuhalalisha ndoa hii haramu(Mut'a)


Hoja kubwa inayotolewa na wale wenye kuhalalisha ndoa hii ya haramu (Shia Ith'naasharia) ni aya ya 24 ya surat al nisaa isemayo;
فما استمتعتم به منهنّ فآتوهنّ أجورهنّ فريضة...) (
(Na ambao mmestarehe nao katika wao,basi wapeni mahari yao yaliyo lazimu...)

kisha husema kwamba wameafikiana wanawachuoni wote kwamba aya hii imeshuka kuhalalisha Mut'a,kisha wanakutajia mirundo ya vitabu vya tafsiri kama kawaida yao ili kuwababaisha wasio jua.
jawabu yetu ni kama ifuatavyo;
a) Aya hii haikuteremka kwa ajili ya kuhalalisha ndoa ya Mut'a,bali aya hii imekuja kuelezea hukumu ya ndoa ya kudumu kwamba iwapo mtawaoa wanawake kisha mkastarehe nao kwa kuwaingilia basi wapeni mahari yao kamili,kwasababu kiislamu ni kwamba mtu akimuoa mwanamke kisha ikatokea kwamba hakuwahi kumuingilia,basi anatakikana mwanamke huyo apewe nusu ya mahari na si mahari kamili,na kama mume atawahi kumuingilia mkewe basi atalazimika kutoa mahari kamili kama inavyoelezea ya hii.
b)kudai kwamba wanawachuoni wameafikiana juu ya tafsiri hiyo,huo ni miongoni mwa urongo wa kishia,na hakuna mwanawachuoni yoyote aliyeelezea maafikiano hayo,si mwanawachuoni wa kishia wala wa Ah'lusunn,bali mambo ni kinyume cha hivyo,bali wanawachuoni wa Ah'lu Sunna wameafikiana kwamba aya hii haizungumzii ndoa ya Mut'a kwa hoja na dalili,tutazija katika sehemu yake.
amesema Imamu Ibin Jarir Twabari baada ya kutaja kauli mbili za wanawachuoni juu ya tafsiri ya aya hii;
(Na tafsiri iliyo bora katika tafsiri mbili hizi,na iliyo sawasawa,ni tafsiri ya mwenye kutafsiri hivi;
Na wale ambao mmewaona katika hao -wanawake- na mkawaingilia,basi wapeni mahari zao.
kwasababu ya kusimama hoja ya  kuharamisha Mwenyezi Mungu kustarehe na wanawake bila ya kutumia njia zilizo sahihi za ndoa,au bila umiliki sahihi,-ameliharamisha hilo- kupitia ulimi wa Mtume wake (s.a.w.)
tazama tafsir Twabari juz 5 uk 19.

Comments :

0 comments to “MU'TA NDOA YA HARAMU”

Post a Comment

 

Website Hit