Islamic Calender

Powered by Blogger.

KAULI ZA WEMA WALIOTANGULIA KUHUSIANA NA BID’AH


Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
Yeyote anayezua au akampokea vizuri mzushi (mtu wa bid’ah) basi juu yake laana ya Allaah, malaika Wake, na ummah mzima [Imepokewa na Al-Bukhaariy (12/41) na Muslim (9/140)]

Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
“Kila jambo la uzushi ni upotofu, hata kama watu wataliona kuwa ni jambo zuri.”
[Imepokewa na Abu Shaamah, uk. 39]


Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) amesema:
“Kwa hakika jambo la kuchukiza zaidi mbele ya Allaah ni mambo ya uzushi”
[Imepokewa na al- Bayhaqiy katika as-Sunan al-Kubraa (4/316)]


Sufyaan ath-Thawriy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Mambo ya uzushi yanampendeza zaidi Shaytwaan kuliko dhambi, kwani mtu hutubia kutokana na madhambi yake lakini hatubii kwa mambo ya uzushi.”
[Imepokewa na al-Laalikaa’iy katika Sharh Uswuul I’tiqaad Ahlis-Sunnah wal-Jamaa’ah (uk. 238)]


Abu Haatim (Rahimahu Allaah) amesema:
“Alama ya watu wa bid’ah ni kule kupingana kwao na watu wapokezi wa riwaya.”
[Imepokewa na al-Laalikaa’iy katika Sharh Uswuul I’tiqaad Ahlis-Sunnah wal-Jamaa’ah Mj. 1, uk. 179]


Sufyaan ath-Thawriy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Yeyote anayemsikiliza mzushi basi atakuwa ameondoka katika hifadhi ya Allaah na amejiunga na mambo ya uzushi.” [Imepokewa na Abu Nu’aym katika al-Hilyah (7/26) na Ibn Battah (na. 444)]


Ibrahiym bin Maysarah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Yeyote anayemtukuza mzushi basi atakuwa amesaidia katika kuuangamiza Uislamu”
[Imepokewa na al-Laalikaa’iy katika Sharh Uswuul I’tiqaad Ahlis-Sunnah wal-Jamaa’ah (1/139)]


Al-Awzaa’iy (Rahimahu Allaah) amesema kuwa:
‘Umar bin ‘Abdil-‘Aziyz (Rahimahu Allaah) amesema:
“Mtakapoona watu wakikutana kisiri kuhusu mambo ya dini juu ya jambo lolote pasi na kuwahusisha watu wa kawaida – basi jueni ya kwamba hao wako katika misingi ya upotofu”
[Imepokewa na al Laalikaa’iy katika Sharh Uswuul I’tiqaad Ahlis-Sunnah wal-Jamaa’ah (uk. 251)]


Al-Hasan al-Baswriy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Msishiriki katika vikao vya watu wa bida'h (uzushi) na (watu) wenye kufuata matamanio yao, wala msibishane nao, wala msiwasikilize.”
[Imepokewa katika Sunan ad- Daarimiy (1/121)]


Al-Fudhayl bin ‘Iyaad (Rahimahu Allaah) amesema:
“Nilikutana na watu walio bora, wote walikuwa ni watu walioshikamana na sunnah na walikuwa wakikataza kuandamana na watu wa bida'h. ”
[Imepokewa na al-Laalikaa’iy katika Sharh Uswuul I’tiqaad Ahlis-Sunnah wal-Jamaa’ah (uk. 267)]


Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Shikamana na Hadiyth na njia ya Salafus-Swaalih (watangulizi wema), na jihadhari na mambo mapya yanayozuliwa, kwani yote hayo ni bid’ah.”
[Imepokewa na as-Suyutiy katika Sawnul Muntaq uk. 32]


Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:
“Yeyote anayeanzisha katika Uislamu jambo la uzushi, na akalidhania kuwa ni zuri, basi huyo amedai ya kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amefanya khiyana katika (amana ya kuufikiliza) ujumbe.”


Amesema tena:
“Uovu ulioje walionao watu wazushi, hatuwapi hata salaam!”
[Imepokewa na al-Baghawiy katika Sharh us-Sunnah (1/234)]


Imaam ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Mtu akutane na Allaah awe amefanya kila aina ya dhambi isipokuwa Shirki tu, ni bora kuliko kukutana na Allaah na ‘Ibaadah yoyote katika bid’ah.”
[Imepokewa na al-Bayhaqiy katika al-I’tiqaad (uk.158)]


Al-Layth bin Sa’ad (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hata kama ningelimuona mtu wa hawaa (mwenye kufuata matamanio ya nafsi – yaani mtu wa bid’ah) anatembea juu ya maji, nisingelimkubali”

Imaam ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaah) aliposikia hayo ya al-Layth, naye akasema:
“Yeye (al-Layth) ameteleza kidogo (katika maneno yake). Mimi hata kama ningelimuona anatembea angani, nisingelikubali chochote kutoka kwake.”
[Imepokewa na as-Suyuutiy katika al-Amr bil 'Ittibaa wan-Nahyi ‘anil Ibtidaa']


Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:
“Katika nguzo muhimu za Sunnah kwetu sisi ni kujiepusha na mambo ya kuzua; na kila jambo la uzushi ni upotofu.”
[Katika kitabu chake Uswuul as-Sunnah uk. 1]

Comments :

0 comments to “KAULI ZA WEMA WALIOTANGULIA KUHUSIANA NA BID’AH”

Post a Comment

 

Website Hit