Islamic Calender

Powered by Blogger.

UMUHIMU WA KIJIFUNZA LUGHA YA QUR-AN:

Ili uweze kuifahamu Qur-aan kama Anavyokusudia Allaah (S.W), hakuna budi kuisoma kwa Lugha yake ya asili kwani Lugha ya Kiarabu ni Lugha pana, yenye ufasaha wa aina ya pekee na ndio maana Allaah (S.W) kwa hikma Yake, Akaichagua Lugha hii kuwa ni Lugha ya Qur-aan na kuituma kwa Mjumbe Mwarabu Muhammad (S.A.W).
 Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) anasema katika aya zifuatato

((Kwa Jina La Allaah, Mwingi Wa Rehma Mwenye Kurehemu Daima))

1.   ((Haa Miym)) ((Naapa kwa Kitabu kinachobainisha)) ((Hakika Sisi tumeifanya Qur-aan kwa Kiarabu ili mfahamu)) [Az-Zukhruf: 1-3]  



2.   Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni(ASH-SHURAA 7)



3.   Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia.(Yusuf 2)


Asiyejua Lugha ya Qur-aan atakuwa ameharamishwa na utamu halisi wa ufahamu wa Qur-aan na Baraka zake
Wala haina tabu kujifunza Lugha hii ya Qur-aan ikiwa mtu atatilia juhudi kwani
Kwa hiyo hakutakuwa na hoja kwa mtu kutokuweza kujifunza Lugha hii tukufu ya Qur-aan na Siku ya Qiyaamah tutakaposimamishwa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuulizwa kwa nini tumeitupa Qur-aan au kwa nini hatukuisoma kwa kuipa haki ya kusomwa kwake, kila mmoja wetu itabidi ajibu swali hili na hatakuwa mtu na kisingizio kuwa hakupata njia za kujifunza Lugha hii ili afahamu kauli na maneno ya Mola wake Mtukufu.

Comments :

0 comments to “UMUHIMU WA KIJIFUNZA LUGHA YA QUR-AN:”

Post a Comment

 

Website Hit