Islamic Calender

Powered by Blogger.

TAMKO LA WAISLAM WA TABORA


                          Bismillah Rahman Rahim

TAMKO LA WAISLAM WA TABORA
 TABORA ndio ilikuwa mkoa mwenyeji mwaka 1958 wakati wa mkutano wa TANU ilioamua TANU kuingia katika uchaguzi wa hila ma ubaguzi dhidi ya Waislam,uchaguzi wa KURA TATU.Kwaq mkutano huo ,mji wa tabora unabeba simamzi kubwa ya kihistoria ya kuwa mkoa ambao kikao kilichofungua milango ya dhulma kwa waislam kwa kuwabagua na kuwaondoa Waislam katika hatamu ya uongozi.

Tunawakumbuka wazee wetu:
·         Bilal Rehani waikela
·         Hamisi nyanya
·         Chamng’anda Usingizi
·         Fimbo Mtwana
·         Rashidi Mussa
·         Mwinyi Hatibu Hemedi
·         Ramadhani Nassibu-Bedui
·         Abdallah Kivuruga
·         Maulid kivuruga
·         Ramadhani   Nasibu
·         Hamisi wabeba
·         Issa Kibira
·         Rajabu Kanyama
·         Mohammed mangiringiri
·         Fundi mhindi
·         Nyange Binti Chande
·         Abedi Kazimoto
·         Jaffar Iddi Songoro
·         Abdallah saidi kasongo(Zani)
·         Iddi Ludete
Na wengine Wengi ambao Juhudi zao Zilisalitiwa na Julius Kambarage Nyerere kupitia MFUMO KRISTO.
Kwa Heshima ileile ya wazee hawa ambao wengi ni marehemu ,Kwa heshiima ya mchango  wao wa mali na nafsi katika kuleta Uhuru wan nchi hii kwa kumuondoa Mwingereza ,Leo sisi watoto na wajukuu wao tumekusanyika hapa ,mbele ya msikiti huu wa Kufungua milango ya kutokomeza mfumo kristo.katika nchi yetu.
Kama wazee wetu waliotoa machozi kwenye mkutano wa hadhara mwaka 1958 na kumshitakia mwingereza kwa mwenyezi mungu(S.W),iwapo angekataa kutoa uhuru wa Tanganyika ,Wakasalitiwa na Yule waliomuamini
Leo hii na sisi tunatoa  tunatoawa machozi tukielekeza dua zetu kwa Allah mbele ya msikiti huu kuwa MFUMO KRISTO katika nchi hii utaondoka kama alivyo ondoka mwingereza Inshallah.
Kwa sababu ya haya yote sisi waislam wa Tabora tunatamka yafuatayo:-
1.   Tunaunga mkono mia kwa mia yote yalioandikwa katika tamko la waislam lililotolewa Diamond Jublee Dar es salaam siku ya jumamosi 15 january 2011,
2.   Tunaunga mkono mia kwa mia yote yalioandikwa katika tamko la waislam lililotolewa Mkoa wa Mwanza jumapili 23 January 2011.
3.   Selikari Iwachukulie hatua za kisheria wale Maaskofu wote  na wale wote waliochochea ghasia za Arusha.
4.   Selikari itoe ufafanuzi wa  kina kwa waislam juu ya tume ya majeshi ya kivita walionayo wakatoliki hapa Tanzania inafanya kazi gani na kwa mujibu wa Sheria gani?
5.   Selikari  iweke  kwenye katiba ya sheria za nchi kuwa ijumaa  ni siku ya mapunziko
6.   Katiba itakayoandikwa itamke waziwazi kuwa nafasi za utendaji Selikarini na Taasisi za umma zitazingatia  uwepo wa waislam na Wakristo.
7.   Tunawaonya maaskofu waache kuivuruga Selikari kwa matamshi yao yaliojaa chuki ya U-dini kwa ni watapelekea amani kuvurugikamkama ilivyokuwa Rwanda mwaka 1994
8.   Uraisi  wa muungano uwe ni wa kupokezana baina ya Bara na  na 2015 ni zamu ya Visiwani
9.   Ipigwe Hesabu ya fedha  ambayo selikari imeyapa makanisa Tangu Uhuru 1961 hadi leo ili na sisi waislam tupate mhao wetu na waliofanya haya washitakiwe
10.                Haya yote yakishindikana na ili tuishi kwa amani ,TUGAWANE NCHI KAMA ILIVYO SUDAN na ,NGERIA

Wabillah Taufiq

(imetolewa katika kongamano lililojadili hali ya waislam na mustaqbal wa  nchi  ya Tanzania.Kongamano hilo lilifanyika Junapili 30 January 2011 katika viwanja vya msiki wa Ijumaa Gongoni ,Tabora.
·          

Comments :

0 comments to “TAMKO LA WAISLAM WA TABORA”

Post a Comment

 

Website Hit